Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imeandaa mfumo wa Takwimu za Elimu ujulikanao kama Education Sector Management Information System (ESMIS). Mfumo huo umeundwa na Wataalamu wa TEHAMA kutoka Wizara hiyo Kwa kushirikiana na Taasisi nyingine ukilenga kuwezesha ukusanyaji, uchambuzi na usimamizi wa takwimu muhimu za sekta ya elimu.



Timu hiyo ya Wataalamu tarehe 18, Septemba 2025 imewasilisha mfumo huo kwa Wakurugenzi wa Wizara ya Elimu ili kutathmini na kutoa maoni ya kuuwezesha kuboreshwa na kuwa toshelezi kwa Takwimu za sekta nzima pamoja na maoni juu utendaji wa mfumo kabla ya kazi ya uandaaji kukamilika.



Aidha, mfumo huo ukikamilika utaongeza ufanisi kwa kuwa na urahisi wa upatikanaji takwimu kwa ajili ya maamuzi na katika usimamizi na uendeshaji wa elimu nchini.