Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi zake ikiwemo Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Baraza la Taifa la Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) imeendelea kutoa elimu juu ya utekekezaji wa Sera na Mitaala iliyoboreshwa.
Leo Mei 2, 2024 jijini Dodoma tumekutana kutoa elimu na kupokea maoni kutoka kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo na Wabunge wabobezi katika masuala ya Elimu (PAQEA) kuhusu utekelezaji huo.