Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema utekelezaji wa agizo la Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan la kuboresha vyuo vya ualimu nchini umeleta mageuzi makubwa katika sekta ya elimu.



Akizungumza Aprili 26, 2026 Mjini Morogoro wakati wa uwekaji jiwe la Msingi katika Chuo Cha Ualimu Dakawa, Prof. Mkenda amesema utekelezaji wa agizo hilo umemwezesha kujengwa upya kwa vyuo vitatu vya ualimu ambavyo ni Mgonda, Kabanga na Sumbawanga



Aidha, vyuo vingine 26 vimeongezewa majengo mapya na kufanyiwa ukarabati mkubwa, ikiwemo Chuo cha Ualimu Dakawa ambacho majengo 11 yamekamilika kwa asilimia 92.