Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo ameongoza ujumbe wa Wizara katika ziara ya Ulinganishaji (benchmaking) nchini India.



Katika ziara hiyo, Prof. Nombo amekutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Umoja wa Vyama vya Vyuo Vikuu nchini India ambapo wamekuabaliana kuingia mashirikiano kati ya Vyuo vikuu vya India na Vyuo vikuu vya Tanzania katika maeneo mbalimbali