Timu ya Maafisa Mawasiliano wa Serikali kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Maendeleo Jamii , Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum na Ofisi ya Rais -TAMISEMI wamekutana mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam kuweka mikakati ya pamoja ya kutangaza shughuli zinazofanywa na Serikali kupitia Mradi wa Uwezeshaji kipitia Ujuzi ,(ESP)



Mradi wa ESP unatekelezwa na Jumuiya ya Vyuo na Taasisi za Ufundi Canada (CICan) kwa ushirikiano wa karibu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mradi huu unafadhiliwa na Serikali ya Canada.



Lengo kuu la mradi huu ni kuboresha Ushiriki wa Wanawake na Wasichana kwenye shughuli za Kiuchumi na unatekelezwa katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC) na Asasi za Kijamii (CBOs) katika Wilaya 12 nchini ili kuongeza kiwango cha Wanawake na Wasichana katika programu za mafunzo ya ujuzi na kuboresha mafunzo ya biashara, ujuzi, jinsia na haki za binafamu katika jamii zao