*PROF. NOMBO ATETA NA USAID UTEKELEZAJI MAGEUZI YA ELIMU*

Na WyEST, Dodoma

Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amefanya mazungumzo na wajumbe kutoka Shirika la Kimarekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) juu ya masuala mbalimbali katika sekta ya elimu nchini Mkutano huo umefanyika Julai 10, 2024 Jijini Dodoma.

Prof Nombo amesema kuwa wizara imeanza utekelezaji wa mageuzi makubwa katika sekta ya elimu baada ya maboresho ya mitaala na mapitio ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014. Katibu Mkuu ameongeza kuwa katika utekelezaji huo suala la ubunifu linapewa kipaumbele na kwamba ipo tayari kushirikiana na yeyote anayekuja na ubunifu katika masuala yote ya ufundishaji na ujifunzaji "Ubunifu wowote unaosaidia katika utkelezaji wa mageuzi ya elimu na ambao unaendana na tamaduni za nchi unapokekewa" amesisitiza

Prof. Nombo Katibu Mkuu amewataka USAID kushirikiana na wataalam wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Ofisi ya Rais TAMISEMI katika kuandaa mradi wao ili uweze kuwa na matakwa ya serikali. Mkurugenzi Mkazi wa USAID Tanzania Dkt. Thomas LeBlanc amemwambia Katibu Mkuu kuwa Shirika lake lipo katika mchakato wa kuandaa Mradi mkubwa wa kibunifu katika kufundisha msingi wa kuwezesha wanafunzi kujifunza Kusoma, Kiandika na Kuhesabu. Dkt. LeBlanc ameongeza kuwa shirika hilo lipo tayari kukaa na wataalam wa serikali katika kuandaa mradi huo.