Mhe.Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ameweka jiwe la Msingi la Ujenzi wa Jengo la Taaluma na Utawala la Taasisi ya Sayansi za Bahari ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Buyu Zanzibar
Hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi imefanyika leo Januari 05, 2025 na kuhudhuria na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dars Es Salam Mhe Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda.
Jengo hilo linajengwa na Serikali kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET) ambao unatekelezwa na Wizara ya Elimu unaolenga katika kuongeza Fursa za Elimu ya Juu nchini na kuchagiza maendeleo ya kiuchumi