Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amesema mabadiliko yaliyofanyika kwenye Sera ya Elimu yamelenga maslahi mapana ya Taifa hivyo jamii inapaswa kupata uelewa wa kutosha juu ya umuhimu wa mabadiliko hayo.

Mhe. Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Bungeni jijini Dodoma wakati akieleza kuhusu kuidhinishwa kwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na mitaala ya Elimu ngazi ya Elimu ya Awali, Msingi Sekondari na Elimu ya Ualimu.

Mhe. Majaliwa amesema maboresho ya Sera hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan aliyoyatoa kwa nyakati tofauti juu ya kufanya mapitio ya Sera ya elimu na Mafunzo ya 2014 pamoja na kufanya maboresho ya mitaala ya elimu katika ngazi mbalimbali ili ijikite katika kutoka elimu ujuzi badala ya elimu ya taaluma pekee.



"Kwa kuzingatia maelekezo hayo serikali inaendelea na maandalizi ya utekelezaji wa sera na mitaala iliyoidhinishwa kwa kuzingatia kalenda" alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha Waziri Mkuu amebainisha kuwa mitaala mipya iliyoidhinishwa imejikita katika kuwajengea wanafunzi Ujuzi stahiki kwa ajili ya soko la ajira, kwani imetoa kipaumbele kwenye stadi za amali katika ngazi zote za Elimu