Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) itatoa Tuzo kwa Walimu walioshinda Shindano la Pili la Stadi za kufundisha Somo la Kiingereza kwa Shule za Msingi.



Halfa ya utoaji Tuzo hizo inafanyika leo Juni 25, 2024 Jijini Dar es Salaam ambapo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda atakabidhi Tuzo hizo kwa washindi.



Shindano hilo linafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji na Ujifunzaji kwa Shule za Awali na Msingi (BOOST).