Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni, na Michezo imeendelea na vikao vya kupokea taarifa kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia
Leo Oktoba 21, 2024 jijini Dodoma Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha taarifa ya Utekelezaji wa Tahasusi mpya za kidato cha tano na ushirikishwaji wa Wadau kwenye uandaaji wa tahasusi hizo
Kikao hicho kimeongozwa na Mhe. Anastazia Wambura na Menejimenti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiongozwa na Mhe. QS Omari Kipanga Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia