Uzinduzi wa Mpango wa Ushirikiano kati ya Taasisi za Elimu na Viwanda unaofanyika leo Februari 9, 2026 jijini Dar es Salaam ni muendelezo wa mageuzi ya elimu yanayokwenda kuunganisha nadharia darasani na vitendo viwandani.



Mpango huu utawezesha kupata Wahitimu watakaokuwa na ujuzi tayari kushiriki katika uchumi wa viwanda.



Ushuhuda huu wa ushirikiano unaonyeshwa na Wadau waliokusanyika JNICC kuwa elimu si jukumu la Serikali pekee, bali ni jukumu la jamii nzima.



Kwa maneno rahisi, tukio hili linaweza kuelezwa kama: "Watu wamekusanyika JNICC kushuhudia historia ikiandikwa, elimu ikipata sura mpya ya ushirikiano na viwanda, sura itakayobadilisha mustakabali wa taifa.