Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula Ameutaka Uongozi unaosimamia Ujenzi wa VETA Ubungo kuongeza ufanisi na juhudi binafsi ili kutatua Changamoto zinazo chelewesha ukamilishwaji wa Ujenzi wa Mradi huo
Ametoa rai hiyo Leo August 30 2023 Alipotembelea kukagua Maendeleo ya Ujenzi wa Mradi huo na kukutana na wasimamizi wa Mradi kuona hatua za awali za ujenzi zinazoendelea na kupewa tathmini fupi ya Ujenzi ulipofikia
Aidha Dkt Rwezimula amewataka wasimamizi wa Mradi huo kuweka kipaumbele cha fursa za kazi kwa vijana wanaozunguka eneo hilo la ujenzi wa Chuo