Naibu Katibu Mkuu, Prof. Daniel Mushi, amesema kuwa zoezi la upandaji miti lililofanyika kwa heshima ya siku ya kuzaliwa ya Rais ni hatua ya kihistoria ya kulinda mazingira na kuacha kumbukumbu ya kudumu kwa vizazi vijavyo.



Akizungumza Januari 27, 2026 Jijini Dodoma katika tukio hilo, Prof. Mushi alisisitiza kuwa lengo la upandaji miti ni kujenga Tanzania ya Kijani na kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi, hususan kupotea kwa uoto wa asili. Alieleza kuwa kipindi cha mvua kimekuwa muafaka kwa kuhakikisha miti iliyopandwa inastawi, huku timu maalum ikihakikisha inamwagilia miti hadi itakapoweza kujisimamia yenyewe.



Aidha, alisisitiza kuwa zoezi hilo linafanyika sambamba na maadhimisho ya siku ya kuzaliwa ya Rais, ambaye ametajwa kuwa mwanamazingira na kiongozi wa kwanza kusimamia masuala ya mazingira kwa dhati.