
Naibu Waziri Mkuu wa Uganda atembelea banda la TCU katika Mkutano wa Mawaziri wa Elimu ya Juu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Naibu Waziri Mkuu wa Uganda, Mhe. Nakadama Rukia Isanga (MB), leo Septemba 10, 2025 ametembelea banda la maonesho la Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) katika Mkutano wa Kwanza wa Mawaziri wa Kikanda kuhuau Elimu ya Juu Kampala Uganda.
Katika banda la TCU, Naibu Waziri Mkuu alipokelewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Daniel Mushi pamoja na viongozi wa TCU akiwemo Mkurugenzi wa Ithibati wa TCU, Dkt. Telemu Kassile.