Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia prof. Adolf Mkenda ametoa wito kwa Bodi ya Waasibu na Wakaguzi wa Heasabu (NBAA) kuanza kuandika vitabu.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam Novemba 10, 2024 baada ya kuhitimisha Matembezi ya Hiari ya kuchangia vitabu vya Sekondari amesema kuwa wahasibu na wakaguzi wa hesabu waandike vitabu vya biashara, Hesabu na _Bookeeping_ na kuvileta kwa Kamishna wa Elimu vipate ithibati na vikiwa na vigezo vitumike shuleni.
Ameongeza kuwa vitabu vikiandikwa na wataalamu wa kada husika vinaweza kuwa na bora zaidi na kwamba serikali inatenga fedha kwa ajili ya kununua vitabu na kuvisambaza katika shule.
Tunahimiza uandishi wa vitabu ili kukuza utamaduni wa kusoma na kuwezesha upatikanaji wa vitabu vya kiada na ziada.
“ Bado hatujafikia lengo la Serikali la kuhakikisha kitabu kimoja cha kiada kwa mwanafunzi mmoja, serikali inaendelea kuwekeza kuhakikisha shuleni kunakuwa na vitabu vya kutosha vya Kiada na Ziada” amesisitiza Prof. Mkenda