
Tukio la Tuzo ya Taifa ya mwalimu Nyerere ya uandishi Bunifu, limeanza na kikao cha awali kilichoongozwa na mgeni maalum, Prof. Ibrahim Noor, ambapo alipata fursa ya kukutana na waandishi wa vitabu kutoka maeneo mbalimbali nchini kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kujadili njia bora za kuboresha sanaa ya uandishi nchini.