Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amekutana na viongozi wa. Umoja wa Wanawake Wamiliki wa Shule na Vyuo( TAWOSCO) ambapo umoja huo wameeeleza kuwa tayari kuendelea kushirikiana na Serikali katika kutelekeleza Sera na Mitaala mipya ya Elimu.



Kikao hicho kilicholenga kujadili mwelekeo mpya wa maendeleo katika sekta ya elimu nchini kefanyika jijini Dar es Salaam tarehe 6 Agosti 2025 kilihudhuriwa pia na Katibu Mkuu Prof Carolyne Nombo, Kamishna wa Elimu Dkt..Lyabwene Mtahabwa, Mtendaji Mkuu wa Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Prof. Said Mohamed Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt Annet Komba