Majengo hayo ni pamoja na madarasa, vyumba vya Mihadhara, maabara, studio na ofisi za walimu ambayo yamefikia asilimia 39 ya ujenzi.
Akiongea Machi 25, 2024 Jijini Dar es Salaam Naobu Katibu Mkuu Prof. James Mdoe amesema ameridhishwa na kasi na hatua iliyofikiwa kwa kuwa ujenzi wa majengo hayo ulianza Mwezi wa Agosti 2023 na kuwataka wakandarasi kuhakikisha wanakamilisha ujenzi huo kwa muda uliopangwa na kwa ubora.
"niwapongeze uongozi wa chuo, wasimamizi na mkandarasi kwa kasi ya ujenzi na ubora , niwaombe kasi hii iendelee" amesema Mdoe.
Mdoe amesema Chuo hicho kupitia mradi wa HEET imepata ufadhili wa Dola za kimarekani milioni 29 ambapo asilimia 70 ya fedha hizo zimeenda kwenye ujenzi katika kmpasi hiyo na Kampasi mpya ya Sengerema.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Ardhi Prof. Evaristo Liwa amemweleza Naibu Katibu Mkuu kuwa majengo hayo yakikamilika yatakuwa na uwezo wa kuhudumia wanafunzi zaidi ya 6,000 na kwamba kwa ujumla ujenzi katika Kampasi hizo mbili utaongeza udahili wa wanafunzi kutoka 6,000 hadi kufikia zaidi ya 15,000.