Mkuu wa Kitengo cha Elimu Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) Dr. Daniel Baheta ameipongeza Serikali ya Tanzania kuona kwamba sera mpya inatambua umuhimu wa elimu katika maisha ya mtu, pamoja kuweka msisitizo wa utoaji wa elimu ya watu wazima kama sehemu ya msingi ya kujifunza kwa watu wote.
Baheta amesema hayo leo 01, Machi 2024 jijini Dar es Salaam wakati akizungumza katika Kongamano la Kitaifa la Elimu Bila Ukomo, ambapo amesema kuwa kasi ya mabadiliko ya kidijiti yanachochea uhitaji wa fursa za kujifunza katika maisha yote na kwamba elimu haiwezi tena kuwekewa kikomo kwa ajili ya kufungua fursa zaidi za ajira na maendeleo ya mtu binafsi.