Serikali imetenga fedha katika Bodi ya Maktaba Tanzania kwa ajili ya ununuzi wa vitabu ili kuwezesha watanzania kupata vitabu na kujenga tabia ya usomaji.
Hayo yameelezwa Agosti 02, 2024 Jijini Dar es Salaam na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof.Adolf Mkenda wakati wa Uzinduzi wa Kitabu cha Riwaya chenye jina *Tangled Web* kilichoandikwa na Euanice Urio.
Prof. Mkenda ameongeza kuwa serikali pia imetenga fedha kwa ajili ya kuchapisha, kununua na kusambaza katika shule na maktaba vitabu vya Washindi wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu
"Serikali bado inahimiza uandishi na usomaji wa vitabu na ndio maana ilianzisha Tuzo ya Kitaifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu ambayo inahusisha uandishi wa riwaya, mashairi, hadithi fupi na za watoto katika lugha ya kiswahili" amesema Waziri wa Elimu.