Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo leo Agosti 28, 2023 Jijini Dodoma amekutana na Watumishi wa Idara ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Kikao hicho kimelenga kufanya majadiliano ya pamoja kuhusu utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya Idara hiyo ikiwa ni pamoja na kufanya tathimini ya Ujuzi unaotolewa na Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi.
Akizungumza katika kikao hicho Prof. Nombo amesisitiza umuhimu wa kuweka utaratibu wa kufanya tathimini kuhusu jukumu mahususi la Idara hiyo ambalo linajikita katika Kukuza na Kuendeleza Ufundishaji na Ujifunzaji, Utafiti na Uvumbuzi.
Pia amewataka Watumishi hao kutafakari na kujiandaa kikamilifu kufuatia Mabadiliko kulingana na Sera ya Elimu na Mitaala inayopendekezwa ili waweze kwenda sambamba na malengo ya serikali katika kuimarisha Mafunzo ya Amali.