
Leo, tarehe 19 Agosti 2025, ujumbe kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar umetembelea Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu, Prof. Carolyne Nombo.
Lengo kuu la ziara hiyo lilikuwa kujifunza namna Elimu ya Watu Wazima pamoja na Elimu nje ya Mfumo Rasmi inavyotekelezwa Tanzania Bara.
Katika mazungumzo hayo, Prof. Nombo aliwaeleza uzoefu wa Tanzania Bara katika kuendesha programu hizo, na kutoa ushauri kuhusu mbinu bora za kuimarisha kuendesha Elimu ya Watu Wazima ufuatiliaji wa matokeo, na ushirikishwaji wa jamii katika utekelezaji wa elimu hiyo
-