Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto (UNICEF) limeipongeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa kukamilisha uandaaji wa Rasimu ya Mkakati wa Matumizi ya Teknolojia za Kijiditali katika elimu.



Pongezi hizo zimetolewa Jijini Dar es Salaam Juni 24,2024 na Mtaalamu wa Elimu kutoka UNICEF Ayoub Kafyulilo ambapo amesema kuwa Mkakati huo unaipeleka elimu kuwa Kijiditali ambapo inashuhudiwa maendeleo ya kijiditali kupitia Maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na juhudi za kuunganisha shule zote na mtandao wa interneti.



"Tunatakiwa kuwaandaa watoto wetu katika ulimwengu wa Kijiditali ambapo masuala mengi ya ujifunzaji yanafanyika kupitia teknolojia, elimu ni nyenzo muhimu ya kuwatayarisha watoto kuwa sehemu ya mabadiliko mapya tunayoyaona" amesema Kafyulilo

 6