Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amezindua shule za Msingi zilizojengwa na Mradi wa kuimarisha Shule za Awali na Msingi (BOOST) katika shule ya Msingi Imbele iliyojengwa katika Manispaa ya Singida mkoani Singida kwa niaba ya shule zote zinazojengwa mradi wa huo.

Dkt. Samia amezindua shule hiyo tarehe 15.10.2023 wakati wa ziara yake mkoani Singida.

Amesema amezindua mradi huu ni kwa niaba ya miradi mingine yote kama hii inayojengwa nchini kote ambayo inasaidia watoto waweze kupata elimu bora.

“Watoto wetu kazi yenu sasa ni kusoma kwa sababu shule nzuri mnazo na utaona kwenye Mradi huu wa BOOST tumejenga kuanzia madarasa ya awali hivyo mtoto akiwa na umri kuanzia miaka 4 apelekwe hapo ili aandaliwe kuanza darasa la kwanza;

Pia ametoa rai kwa Wazazi na walezi wote kuhakikisha kuwa watoto wenye umri wa kwenda shule wanapelekwa shule na wanasoma mpaka kumaliza masomo yap pia ameitaka jamii kuitunza miradi hiyo ili iweze kunufaosha na vizazi vijavyo.



Mradi wa BOOST unatekelezwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Ofisi ya Rais -Tamisemi na kufadhiliwa na Benki ya ya Dunia ulianza mwaka 2021 unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano na utagharimu shilingi Trilioni 1.5 pamoja na ujenzi wa miundo mbinu unahusisha pia mafunzo ya Walimu na Wakuu wa Shule.

kwa mwaka huu wa fedha shule mpya za msingi 302 zinajengwa, vyumba vya madarasa 2,929, madarasa ya Awali 368, matundu ya vyoo 5,131, nyumba za Walimu 41, mabweni na majengo ya Utawala 302.

Kufikia september,2023 shilingi Bil. 230 zimetolewa na shule za msingi zilizokamilika 194, madarasa ya awali 364, madarasa ya shule za msingi 2,303