Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga leo Februari 22, 2024 ameshiriki hafla ya utiaji saini ya ujenzi wa majengo 21 ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yatakayojengwa mkoani Dar es Salaam, Lindi na Zanzibar pamoja na utiaji saini mkataba wa usimamizi wa ujenzi wa majengo mengine manne yatakayojengwa mkoani Kagera.Halfa hiyo hiyo iliyoambatana na upokeaji wa vifaa kwa ajili ya Kituo cha kuzalisha na kusambaza Teknolojia cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, imehudhuriwa na Mkuu wa Chuo hicho Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Viongozi mbalimbali.Vifaa vilivyopokelewa na majengo yanayotarajiwa kujengwa ni matokeo ya utekelezaji wa Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi katika Elimu ya Juu HEET ambayo Chuo hicho kinatekeleza.