Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, ameongoza kikao cha kwanza cha Kamati Tendaji ya mradi wa uunganishaji Shule na Intaneti (GIGA) kilichofanyika Wizara hiyo
Mji wa Serikali Mtumba, Dodoma.



Kikao hicho kimejadili maendeleo ya utekelezaji wa Mradi wa GIGA, ambapo Prof. Nombo alipokea taarifa ya utekelezaji wa awali na changamoto zilizopo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuhakikisha shule zinapata huduma ya intaneti kwa ajili ya kuimarisha ujifunzaji wa kidijitali.



Aidha, Kamati hiyo imeidhinisha rasmi Mpango Kazi wa GIGA kwa mwaka wa fedha 2025/2026, ambao unalenga kuongeza kasi ya uunganishaji wa shule