Tanzania na India zakubaliana kushirikiana katika kuandaa nguvu kazi yenye ujuzi unaohitajika katika nchi zote mbili kupitia elimu ya Ufundi na Ufundi stadi.
Makubaliano hayo yamefanyika Januari 14, 2025 nchini India kati ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Ujuzi na Ujasiriamali nchini India Dkt. Abhay Sinha.