Serikali imewekeza zaidi ya shilingi bilioni nne kuboresha miundombinu ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sekondari (SEQUIP). Fedha hizi zimetumika kujenga majengo mapya 11 na kukarabati miundombinu katika mikoa sita, ikiwemo Dar es Salaam, Morogoro, na Mwanza.


Hayo yamesemwa leo, Desemba 12, 2024, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Carolyne Nombo, kwenye Mahafali ya 63 ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.

Prof. Nombo amepongeza Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) kwa kuendelea kutoa elimu bora inayoendana na mabadiliko ya sera ya elimu na teknolojia ili kuandaa wahitimu wenye ujuzi
unaokidhi mahitaji ya jamii.