Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amekutana na Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba kujadili utekelezaji wa bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025 kwa fedha za Serikali na zile za washirika wa maendeleo.
Kikao hicho kimefanyika hii leo Desemba 13, 2024 Katika Ofisi za Wizara ya Fedha zilizopo jijini Dar es Salaam kimehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Pro. Carolyne Nombo na Katibu Mkuu Fedha Dkt Natu El- Maamry Mwamba pamoja na waratibu wa Miradi inayotekelezwa na Wizara na maafisa waandamizo kutoka Wizara ya Fedha
Aidha Waziri Mkenda na Mwigulu wamejadili kuhusu maandalizi ya miradi itakayofadhiliwa na washirika wa maendeleo ya elimu kwa miaka ijayo