Katika Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi vyote 54 Serikali kwa kushirikiana na Wadau imejenga madarasa ya watoto wadogo kwa malengo makuu mawili ikiwemo mafunzo pamoja na kutoa huduma ya malezi kwa watoto wa wanafunzi waliorejea na kuendelea na masomo baada ya kujifungua na kuacha shule.



Zaidi ya wanafunzi 1,138 wanaendelea na elimu ya sekondari katika vyuo hivyo kupitia mpango wa Elimu Haina Mwisho ambapo pia wanasoma masomo ya fani za amali wanazochagua