Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda leo Septemba 20, 2024 ameongea na wananchi wa Kata ya Makowo mkoani Njombe baada ya kuweka jiwe la Msingi la ujenzi wa shule ya Sekondari Makowo.
Prof. Mkenda ameanza ziara ya mkoani Njombe ya kutembelea na kukagua Miradi ya Maendeleo inayotekelezwa mkoani humo ambapo katika siku ya kwanza ya ziara mbali ya kuweka jiwe la msingi katika shule hiyo pia ametembelea na kukagua eneo itakapojengwa kampasi ya Chuo Kikuu cha Dodoma na barabara ya mabatini
Prof. Mkenda amewapongeza wakazi wa Kata ya Makowo na Njombe kwa kuchangia na kuanzisha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo kuchangia ujenzi wa shule, mabweni na vituo vya afya na kuwahakikishia kwamba serikali itaendelea kuunga mkono jitihada hizo.
0