Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf F. Mkenda (Mb), leo tarehe 7 Juni, 2025, ameshiriki ibada ya mazishi ya kumuaga Marehemu Mzee Silvin Ibenge Emanuel Mongella.



Ibada hiyo imefanyika nyumbani kwa marehemu katika Kijiji cha Kabusungu, Wilaya ya Ilemela, Jijini Mwanza na kuhudhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali, wakiongozwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mhe. Balozi Dkt. Emanuel Nchimbi.