Mtanzania Mariam Mhina kutoka kampuni ya TAI Impact Tanzania ameshinda nafasi ya pili kwenye tuzo za ubunifu kwenye Elimu katika Africa Skills Week iliyofanyika Accra Ghana 14 - 18 Oktoba 2024.

Mariam Mhina aliingia katika mashindano yaliyohusisha wabunifu 611 kutoka nchi mbalimbali za Afrika na kufuzu kufikia kwenye wabunifu 10 bora na kwenda kushinda nafasi ya pili.



Hafla ya utoaji tuzo hizo imehudhuriwa pia na Dkt. Fredrick Salukele - Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi na Mafunzo ta Ufundi Stadi katika Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Kongole kwa Mariam Mhina na tunajivunia ushindi huu