Mkuu wa Kitengo cha Sheria Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Adv. Innocent Mgeta amesema Serikali ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023, hivyo inaendelea kushirikisha wadau mbalimbali kufanya mapitio ya Sheria ya Elimu kuwezesha ufanisi katika utekelezaji wake.



Mgeta ameeleza hayo Oktoba 30, 2024 jijini Dar es Salaam akizungumza mbele ya Kamati ya Mapitio ya Sheria ya Elimu na wadau mbalimbali wa maendeleo waliokutana jijini Dar es Salaam kutoa maoni mbalimbali.



Amesisitiza kuwa wadau hao ni muhimu kwa taifa na wana jukumu la kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni kuhusiana na changamoto zilizopo kwenye Sheria ya Elimu Sura ya 353