
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Wanu Hafidh Ameir amewasili katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Chemba kwa ajili ya kukabidhi vifaa vya kufundishia na kujifunzia kwa VETA za Wilaya.

Mhe. Wanu Ameir ameelezwa kuwa katika mwaka wa fedha 2025/26 tayari Wilaya hiyo imeshapokea Shilingi bilioni 1.83 kwa ajili ya sekta ya elimu ikiwemo ujenzi wa miundombinu.


