Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia leo Julai 03, 2024 inetoa Tuzo ya Shukrani kwa Shirika la Maendeleo la Ubelgiji (ENABEL) kwa kudhamini Wiki ya Elimu Ujuzi na Ubunifu Mwaka 2024 iliyofanyika Mkoani Tanga Mwezi Mei.



Tuzo hiyo imekabidhiwa Jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Profesa Carolyne Nombo ambae amewashukuru kwa ufadhili huo pamoja na ufadhili miradi ya elimu Mkoani Kigoma.



Aidha amewaomba kuangalia jinsi ya kuendelea kushirikiana katika kuongeza wigo wa ufadhili wa miradi ili kufikia mikoa mingine huku akisisitiza umuhimu wa kuhakikisha miradi hiyo inaendana na mwelekeo mpya ya Elimu kufuatia uboreshaji wa Sera na Mitaala.



kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika hilo Koene Goekint ameishukuru Serikali kwa kutambua mchango wao na kuahidi kuendeleza ufadhili wa miradi mbalimbali ya elimu kulingana na mahitaji yatakayo ainishwa na Serikali.