
Mawaziri kutoka nchi 19 barani wameshiriki kikao Ministerial Roundtable katika Kongamano la 18 la e-Learning Africa 2025 lililoanza Aprili 7, 2025 JNICC jijini Dar es Salaam.
Kikao hicho linalenga kujadili mikakati mbalimbali ikiwemo kuandaa rasilimaliwatu yenye maarifa na ujuzi pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia za kidijitali katika sekta mbalimbali hususan elimu.