Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea na dhamira ya kukuza ujuzi kwa vijana wa kitanzania Kwa sababu wao ndio nguvu kazi ya Taifa.

Rais Samia ametoa kauli hiyo hii leo Oktoba 17, 2023 katika Viwanja vya Barafu wilayani Igunga baada ya kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa Chuo cha Ufundi Stadi kilichopo wilayani humo mkoani Tabora.

"Chuo hiki ni mwendelezo wa jitihada za Serikali ili kuhakikisha vijana wetu wanapata Mafunzo ya amali, wanapata Elimu ya Ufundi, inayokwenda kuwasaidia kuajiriwa au kujiajiri" alisema Rais Samia.

Ameongeza kuwa Serikali imeamua Wilaya zote nchini kuwa na Vyuo vya Veta ikilenga kufundisha Elimu ya amali, ikizingatia agenda ya Jenga Kesho iliyobora.

"Tuna Miradi mingi nchini, lakini vijana wetu hawapati fursa za ajira kutokana na kukosea umahiri katika fani hisika, wageni wanachukua nafasi huku wakiwaacha vijana wetu" alielesa Mhe. Rais

Katika kutilia mkazo nia ya Serikali ameongeza kuwa "mfano Chuo cha Igunga kinaenda kuzalisha mabigwa na mafundi katika masuala ya Elimu, kilimo na ufugaji.



Kwa Upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amemshukuru Mhe. Rais kuweka jiwe la msingi, kwani kwa hatua hiyo sasa Chuo hicho kitaanza kutoa Mafunzo ya amali kwa vijana wa Igunga na wengine kutoka sehemu mbalimbali za nchi.

Ameeleza kwamba, wizara imefanyia utekelezaji agizo la Mhe. Rais Samia la kuangalia namna ya kuwezesha upatikanaji wa Mikopo kwa Wanafunzi wanaotaka kusoma ngazi ya diploma.

"tumefungua dirisha la kuomba Mikopo, ya kuweza kukopeshwa fedha ya Serikali Kusoma katika ngazi ya diploma. Naomba wazazi na Wanafunzi waangalie kwenye tovuti ya Bodi ya Mikopo wafuate taratibu zote" alufafanua Mkenda.

Nae Mkuu wa mkoa wa Tabora Balozi Batilda Buriani ameishukuru Serikali kwa kutekeleza kwa vitendo Ujenzi wa vyuo vya Veta ili kuchagiza Maendeleo kiuchumi