Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda, Katibu Mkuu Prof. Carolyne Nombo na Naibu Katibu Mkuu Dkt. Franklin Rwezimula leo Julai 23, 2024 Jijini Dodoma wamekutana na kumuaga Mkuu wa kitengo cha Elimu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia watoto (UNICEF) Bw. Daniel Baheta anayetarajia kuondoka nchini Tanzania mwishoni mwa Mwezi Agosti baada ya kupata uhamisho wa kikazi kuelekea nchini Sudani.



Prof Mkenda amemshukuru Baheta kwa kushirikiana na Wizara katika kutekeleza miradi na mipango mbalimbali ya sekta ya elimu na kuhakikisha zinasonganmbele



Aidha Waziri ameongeza kuwa imekua ni heshima kwake na kwa Wizara kufanya kazi naye



"Tutakukumbuka sana,Tanzania ni nyumbani kwako tuzidi wasiliana kokote utakapokua" amesisitiza Prof. Mkenda.



Baheta amesema kuwa anashukuru kwa ushirikiano alioupata nchini Tanzania kwani amefanya kazi ya kuitumikia sekta ya elimu kwa miaka mitano na kwamba amekuwa miongoni mwa familia ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.