Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema kuwa katika mitaala iliyoboreshwa ufundishaji wa masomo ya lugha umeboreshwa.
Prof. Nombo amesema hayo Juni 25, 2024 jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya utoaji Tuzo kwa walimu walioshinda shindano la pili la stadi za kufundisha somo la Kingereza kwa Shule za Msingi.
Prof. Nombo ameongeza kuwa katika kuimarisha ufundishaji masomo hayo, somo la lugha ya Kiingereza litaanza kufundishwa Darasa la Kwanza kwa shule zinazotumia Kiswahili na somo la Kiswali likianza kufundishwa kuanzia Darasa la Kwanza kwa shule zinazotumia Kiingereza pia.
"Lakini pia mbinu za ufundishaji wa masomo ya lugha zimeboreshwa na zimekuwa ni zile zinazozingatia ujenzi wa umahiri katika kukuza stadi za Kusikiliza, Kuandika, Kuongea na Kusoma" amesisitiza Prof Carolyne Nombo.