NA WyEST
Dar es Salaam
Utekelezaji wa Mradi wa Kujenga Ujuzi na Ushirikiano Afrika Mashariki (EASTRIP) umeiwezesha Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (,DIT) kuongeza udahili wa wanafunzi kutokana 800 hadi kufikia 1500.
Akizungumza Novemba 13, 2024 Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara ya Timu kutoka Benki ya Dunia na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia iliyokuwa ikikagua maendeleo ya Mradi huo, Mratibu wa Mradi Dkt. Joseph Matiku amesema kuwa tangu kuanza kwa mradi huo Mwaka 2018 Taasisi imeongeza udahili maradufu.
Mratibu huyo amesema kuwa udahili umeongezeka kutokana na mradi kuwezesha ujenzi wa miundombinu, uanzishwaji wa programu za mpya 20 za mafunzo na nyingine kufanyiwa maboresho ili ziendane na utoaji wa mafunzo ya ujuzi kulingana na mahitaji ya soko la ajira.
Dkt. Matiko ameongeza kuwa Mradi huo pia umewezesha Taasisi hiyo kuwa na mashirikiano ya Kikanda ambapo wamekuwa wakibadilisha wanafunzi na walimu kutoka nchi moja kwenda nyingine kwa lengo la kubadilishana uzoefu na kwamba wanafunzi wapato 20 kutoka katika Taasisi hiyo walikwenda kujifunza katika vyuo vya nchini kenya na kenya pia ilileta wanafunzi 20 kwa programu ya mafunzo kwa zaidi ya mwezi.
Aidha, Mtatibu huyo ameendelea kuelezea namna Mradi huo ulivyowezesha mashirikiano kati ya DIT na viwanda ambapo katika mashirikiano hayo wameweza kupata maabara tatu zinazowezesha kutoa mafunzo kwa vitendo kwa wanafunzi pamoja na wanafunxo na wakufunxi kupata uzoefu kwa vitendo katika viwanda.
Mkurugenzi wa Elimu ya Ufundi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Fredrick Salukele amesema kuwa Mradi wa EASTRIP unalenga katika kuongeza udahili, ubora wa mafunzo ya ufundi, kuongeza ushiriki wa wanafunxi wa kike katika ptogramu za ufundi, kujenga mashirikiano kati ya Taasisi za Elimu ya Ufundi na Sekta binafsi na kujenga mashirikiano ya kikanda.
Ameongeza kuwa unatakelezwa katika nchi tatu za Afrika Mashariki ambazo ni Kenya, Ethiopia na Tanzania na kwamba Tanzania inajenga vituo vya Umahiri vinne katika vyuo vya ufundi vitatu.
Amevitaja vyuo hivyo kuwa ni Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kinajenga Kituo cha Umahiri katika Nishati Jadidifu, Chuo Taifa cha Usafirishaji (NIT) Kituo cha Umahiri katika Masuala ya Anga na Usafirishaji, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam (DIT) Kampasi ya Dar es Salaam inayojenga Kituo cha Umahiri katika Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na DIT Kampasi ya Mwanza inajenga Kituo cha Umahiri katika Mazao ya Ngozi.