Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Bw. Khamis Abdulla Said amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imegharamia kwa asilimia miamoja mradi wa ujenzi wa Skuli ya Sekondari Kizimkazi Dimbani iliyopo Kisiwani Unguja kwa kutumia fedha za direct indicators, ambapo jumla ya shilingi Milioni 223 zimetumika.



Katibu Mkuu huyo ameeleza hayo Agosti 24, 2024 wakati wa Uzinduzi wa Skuli hiyo, akitoa maelezo kuhusu utekelezaji wa mradi huo, amesema Skuli hiyo ina madarasa manne, chumba cha maabara na maktaba, ofisi ya Mwalimu Mkuu na Ofisi ya Walimu na kwamba itakuwa na uwezo wa kutoa Wanafunzi 180 kwa wastani wa Wanafunzi 45 kila darasa.