Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekitaka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) kitakapokamilisha ujenzi wa Kampasi ya Rukwa kutoa mafunzo kwa vijana wa mkoa wa Rukwa ya namna ya kutumia rasilimali zinazopatikana katika mkoa huo.



Rais ametoa wito huo Julai 17, 2024 wakati alipofika katika Kampasi hiyo kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi ambapo amesema kuwa mkoa huo una rasilimali ya udongo ambayo inaweza kutumika kutengeneza matofali.