Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe amewasili Chuo Kikuu Ardhi jijini Dar es Salaam tayari kufungua Mdahalo wa Nane wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Afrika Mashariki kuhusu uhusiano wa Kikanda.



Mdahalo huo unaofanyika Machi 25, 2024 umeandaliwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki na kufadhiliwa na Umoja wa Ulaya (European Union)