
Mkutano wa Mwaka wa Tathmini ya Pamoja ya Sekta ya Elimu 2024/25 umeingia katika siku yake ya pili Oktoba 23, 2025 jijini Dodoma, ambapo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imewasilisha taarifa ya utekelezaji wa sekta ya elimu kwa mwaka 2024/25.

Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Carolyne Nombo, ameongoza majadiliano kuhusu taarifa hiyo muhimu, yenye lengo la kuboresha ubora wa elimu nchini na kuhakikisha malengo ya maendeleo ya sekta yanatekelezwa kwa ufanisi.

Washiriki wamejadili kwa kina mikakati ya kuimarisha elimu katika ngazi zote kuanzia Elimu ya Awali hadi Elimu ya Juu, sambamba na eneo la sayansi, teknolojia na ubunifu kama nyenzo kuu za kuchochea maendeleo ya taifa na kujenga uchumi wa viwanda


