Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula ameutaka Uongozi wa Chuo cha VETA Chang'ombe kuendeleza Jitihada za kutoa elimu bora ya Ufundi stadi kwa Vijana na kusaidia kupunguza wimbi la vijana wasio na Ajira mitaani.

Ametoa Rai Leo Septemba 1, 2023 alipofika Chuoni hapo na kukutana na Uongozi wa Chuo hicho na kuwaasa kujipanga na kuendana na Mageuzi ya Sekta ya Elimu kwa Kufundisha fani zenye fursa kubwa ya ajira.



Pia Dkt. Rwezimula amekitaka Chuo hicho kuwa na ushirikiano na Taasisi zingine ili kutengeneza mazingira mazuri kwa wanafunzi kipindi cha kwenda kujifunza kwa Vitendo waweze kupata Ujuzi wa ziada utakao wasaidia kufikia malengo yao