Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizungumza na Wahariri wa Vyombo vya Habari juu ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 na Mitaala mipya ya Elimu ya awali msingi sekondari na Ualimu.



Prof. Mkenda amewaeleza Wahariri wao kuwa serikali imeanza kutekeleza Sera na Mitaala hiyo kwa baadhi ya ngazi za elimu huku akisisitiza kuwa utekelezaji huo unafanywa kidogo kidogo ili kuhakikisha unakuwa na mafanikio.



Aidha, ameongeza kuwa ifikapo Mwaka 2027 watakaokuwa darasa la sita na wale wa darasa la saba watamaliza elimu ya msingi kwa wakati mmoja na kufanya makundi mawili kuingia elimu ya sekondari kwa wakati mmoja na hapo ndipo itakapoanza elimu msingi kuwa ya miaka kumi.