Wadau wa Maendeleo wanaoshiriki mkutano wa kutoa maoni kwenye rasimu ya Mapitio ya Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Elimu unaofanyika jijini Dar es Salaam.



Akizungumza katika Mkutano huo Mwenyekiti wa kundi la wadau wa Maendeleo na Mkuu wa Kitengo cha Elimu UNESCO Faith Shayo amesema kuwa Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu ni muhimu kwa kuwa unatoa dira katika maeneo na nyaja mbalimbali ambazo ni vipaumbele vya serikali ambavyo vinawezesha wadau kushiriki katika hatua za maendeleo.



Ameongeza kuwa amefurahishwa kuona Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ilivyoweza kushirikisha wadau kutoka maeneo mbalimbali ikiwemo wanafunzi wa Msingi na Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Juu na Kati katika mkutano huo.



"Mpango wa Maendeleo ya Sekta ya Elimu ni wetu sote na nina furaha kuona pia umekuwa shirikishi hivyo unawapa wadau mbalimbali nafasi kuuangalia, kuuelewa na kutoa maoni ili utuongoze kwa miaka mitano tukiwa na uelewa na bia moja," amesisitiza Shayo