
Benki ya NMB imeahidi kuendelea kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia katika kuimarisha mafunzo ya Sayansi na Teknolojia na uendelezaji vijana wabunifu nchini.

Hayo yameelezwa Machi 10, 2026 Jijini Dodoma na na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya NMB Prof Sylvia Temu ambae aliongoza ujumbe wa viongozi waandamizi wa Benki hiyo katika kikao na uongozi wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.


