Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekagua maendeleo ya ujenzi wa karakana za kufundishia wanafunzi wanaosoma Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) zinazojengwa kupitia Mradi wawa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET)



Mradi wa HEET unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kuboresha mazingira ya kufundishia, kujifunzia na kuboresha mitaala ya Taasisi za Elimu ya Juu ili iendane na mahitaji ya soko la ajira na kuimarisha mfumo wa usimamizi wa Elimu ya Juu nchini.



Mradi wa HEET unagharimu Dola za Marekani milioni 47.5 na unatekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2021 hadi 2026.

109-